Mbeya City kambini Ruvuma, kuivaa Majimaji

Dar es Salaam.
 Timu ya Mbeya City imekwenda Songea mkoani Ruvuma ambako itapiga kambi kujiandaa na mechi zilizosalia za Ligi Kuu.
Baada ya kumrudisha kundini kocha wao, Juma Mwambusi aliyetangaza kujiuzulu hivi karibuni, timu hiyo imekwenda Songea kuweka kambi maalumu na mazoezi ikiwamo kujipima kwa Majimaji ya huko ili kupima nguvu na uwezo wa wachezaji wao.
Aidha, Mbeya City inataka utulivu ili kutatua matatizo yao mbalimbali yaliyosababisha timu hiyo ifanye vibaya kwenye mechi saba zilizopita za Ligi Kuu.
Timu hiyo ilifanya vizuri msimu uliopita na watu wengi kuitabiria kuwa ingetisha msimu huu, imejikuta katika michezo saba iliyocheza ikishinda mmoja, ikatoka sare miwili na kupoteza mingine minne na hivyo kushika mkia.
Mwambusi aliliambia gazeti hili jana kuwa wanakwenda Songea kuweka kambi ya muda na watafanya mazoezi na kucheza na kucheza mechi za kirafiki ili kujiweka sawa.
“Tunakwenda Songea leo (jana) kuweka kambi najua huko tutaweza kufanya mazoezi mazuri na kwa utulivu ili kurudisha ubora wetu wa msimu uliopita.
“Hatujui tutakaa huko hadi lini, viongozi wenyewe ndiyo wanajua lakini tutatumia kambi hii kufanya mazoezi, pia kucheza michezo ya kirafiki na tunaamini hadi tukirudi timu itakuwa katika hali nzuri,” alisema Mwambusi.
Ikiwa Songea, Mbeya City inatarajia kushuka dimbani dhidi ya Majimaji ya Songea inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, kama moja ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji