Mambomu manane yaokotwa Kigoma
Mambomu
manane yaokotwa Kigoma
Watu wawili waliokuwa wikichimba kifusi katika nyumba iliyokuwa ya
diwani wa kata ya mabamba kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya waganga ya kituo cha
afya mabamba wilaya ya kibondo mkoa wa kigoma. waliokota mabomu nane
yanayosadikiwa kuwa yalifukiwa ardhini kwa zaidi ya miaka 10 katika eneo hilo
Mmoja wa wananchi hao waliokuwa wakichimba na kusogeza kifusi cha
udongo ikiwa ni mwendelezo
wa ujenzi wa nyumba ya mganga katika kituo cha afya mabamba Bw fotunatus
katabalo amesema kuwa yeye na mwenzake waliona vitu kama vyuma ambavyo
walivitilia mashaka na kumjulisha
msimamizi wa ujenzi ambaye nae alichukua jukumu la kutaarifu uongozi wa
kata na mkuu wa kituo cha
polisi mabamba kwa ajili ya utambuzi wa vitu hivyo kwani tayari baadhi ya watu
walioviona walikwisha tambua kuwa ni mabomu
Msimamizi wa ujenzi wa nyumba hiyo ya mganga katika kituo cha afya
mabamba bw flansisi petro alisema kuwa yeye alitaarifiwa na watu waliokuwa
wakifanya kazi ya uchimbaji wa msinngi kwa ajili ya ujenzi ndipo naye aliamua
kutaarifu uongozi wa kata kasha kutaarifu polis
Pamoja ni kwamba mabomu si kitu cha kukimbiia lakini mamia ya watu
walifika kujionea tukio hilo na haya ndio
yalikuwa maoni yao
Kwa mujibu wa mtaalamu wa mabomu kutoka kambi ya jeshi iliyoko
kata ya kizazi bw damas Nyitambe amesema kuwa mabomu hayo huenda yamewekwa
kadtika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 10 kwa kuwa yameonekana kuwa na kutu na
kwamba kama moja lingelipuka basi yote yangeweza kulipuka na kusababisha madhara
makubwa na hapa anatoa elimu kwa mamia ya watu waliofika kujionea mabomu hayo
bila kujali kuwa ni hatari kwa maisha yao
Kwa upende wake mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilayani kibondo
bw Venance mwamoto baada ya mamia ya watu kukfika mahali hapo ili kuona mabomu
hayo amewataka wananchi kuwa makini na kutopenda kushangaa vitu vya hatari kama hivyo kwani yangeweza kulipuka na kusababisha maafa
makubwa kutokana na umati mkubwa uliofika kushangaa
Ni mara nyingi kumekuwepo na upatikanaji wa mabomu katika maeneo
mengi ya wilaya za kaonko na kibondo na mkoa mzima wa kigoma hali inayosadikiwa
kuwa uenda yaliachwa na wakimbizi wan chi za Burundi Kongo Na Rwanda walioingia
hapa nchini wakikimbia mapigano katika nchi zao
Kwakuwa wilaya hizo zinapakana
na nchi hizo na walikuwa wakiishi katika baadhi ya vijiji vya wilaya
hizo
Maoni
Chapisha Maoni